Psalms 148
Mwito Kwa Ulimwengu Kumsifu Mungu
1 aMsifuni Bwana.Msifuni Bwana kutoka mbinguni,
msifuni juu vileleni.
2 bMsifuni, enyi malaika wake wote,
msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.
3 cMsifuni yeye, enyi jua na mwezi,
msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.
4 dMsifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana,
na ninyi maji juu ya anga.
5 eVilisifu jina la Bwana
kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.
6 fAliviweka mahali pake milele na milele,
alitoa amri ambayo haibadiliki milele.
7 gMtukuzeni Bwana kutoka duniani,
ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,
8 humeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu,
pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,
9 ininyi milima na vilima vyote,
miti ya matunda na mierezi yote,
10 jwanyama wa mwituni na mifugo yote,
viumbe vidogo na ndege warukao,
11 kwafalme wa dunia na mataifa yote,
ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,
12wanaume vijana na wanawali,
wazee na watoto.
13 lWote na walisifu jina la Bwana,
kwa maana jina lake pekee limetukuka,
utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.
14 mAmewainulia watu wake pembe, ▼
▼Pembe hapa inawakilisha mwenye nguvu, yaani mfalme.
sifa ya watakatifu wake wote,
ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake.
Msifuni Bwana.
Copyright information for
SwhNEN