Psalms 31
Maombi Na Sifa Kwa Kuokolewa Kutoka Kwa Adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 aEe Bwana, nimekukimbilia wewe,usiache nikaaibika kamwe,
kwa haki yako uniokoe.
2 bNitegee sikio lako,
uje uniokoe haraka;
uwe kwangu mwamba wa kimbilio,
ngome imara ya kuniokoa.
3 cKwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu,
uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.
4 dUniepushe na mtego niliotegewa,
maana wewe ndiwe kimbilio langu.
5 eNinaikabidhi roho yangu mikononi mwako,
unikomboe Ee Bwana, uliye Mungu wa kweli.
6 fNinawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili;
mimi ninamtumaini Bwana.
7 gNitafurahia na kushangilia upendo wako,
kwa kuwa uliona mateso yangu
na ulijua maumivu ya nafsi yangu.
8 hHukunikabidhi kwa adui yangu
bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi.
9 iEe Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida;
macho yangu yanafifia kwa huzuni,
nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko.
10 jMaisha yangu yamedhoofika kwa majonzi,
naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali;
nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso,
na mifupa yangu inachakaa.
11 kKwa sababu ya adui zangu wote,
nimedharauliwa kabisa na jirani zangu,
hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho,
wale wanionao barabarani hunikimbia.
12 lNimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa,
nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika.
13 mKwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi;
vitisho viko pande zote;
kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu,
na kula njama kuniua.
14 nLakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana;
nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.”
15 oSiku za maisha yangu ziko mikononi mwako,
uniokoe mikononi mwa adui zangu
na wale wanifuatiao.
16 pMwangazie mtumishi wako uso wako,
uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma.
17 qUsiniache niaibike, Ee Bwana,
kwa maana nimekulilia wewe,
bali waovu waaibishwe
na kunyamazishwa Kuzimu.
18 rMidomo yao isemayo uongo na inyamazishwe,
kwa maana kwa kiburi na dharau
wao husema kwa majivuno
dhidi ya wenye haki.
19 sTazama jinsi ulivyo mkuu wema wako,
uliowawekea akiba wakuchao,
ambao huwapa wale wakukimbiliao
machoni pa watu.
20 tUnawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako
kutokana na hila za wanadamu;
katika makao yako huwaweka salama
kutokana na ndimi za mashtaka.
21 uAtukuzwe Bwana,
kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu
nilipokuwa katika mji uliozingirwa.
22 vKatika hofu yangu nilisema,
“Nimekatiliwa mbali na macho yako!”
Hata hivyo ulisikia kilio changu
ukanihurumia nilipokuita unisaidie.
23 wMpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote!
Bwana huwahifadhi waaminifu,
lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.
24 xKuweni hodari na mjipe moyo,
ninyi nyote mnaomtumaini Bwana.
Copyright information for
SwhNEN