Psalms 40

Wimbo Wa Sifa

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 aNilimngoja Bwana kwa saburi,
naye akaniinamia, akasikia kilio changu.
2 bAkanipandisha kutoka shimo la uharibifu,
kutoka matope na utelezi;
akaiweka miguu yangu juu ya mwamba
na kunipa mahali imara pa kusimama.
3 cAkaweka wimbo mpya kinywani mwangu,
wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa
na kuweka tumaini lao kwa Bwana.

4 dHeri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,
asiyewategemea wenye kiburi,
wale wenye kugeukia miungu ya uongo.
5 eEe Bwana Mungu wangu,
umefanya mambo mengi ya ajabu.
Mambo uliyopanga kwa ajili yetu
hakuna awezaye kukuhesabia;
kama ningesema na kuyaelezea,
yangekuwa mengi mno kuyaelezea.

6 fDhabihu na sadaka hukuvitaka,
lakini umefungua masikio yangu;
Au: bali mwili uliniandalia.

sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi
hukuzihitaji.
7 hNdipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja:
imeandikwa kunihusu katika kitabu.
8 iEe Mungu wangu,
natamani kuyafanya mapenzi yako;
sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”

9 jNimehubiri haki katika kusanyiko kubwa,
sikufunga mdomo wangu,
Ee Bwana, kama ujuavyo.
10 kSikuficha haki yako moyoni mwangu;
ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako.
Sikuficha upendo wako na kweli yako
mbele ya kusanyiko kubwa.

11 lEe Bwana, usizuilie huruma zako,
upendo wako na kweli yako daima vinilinde.
12 mKwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka,
dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.
Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,
nao moyo unazimia ndani yangu.

13 nEe Bwana, uwe radhi kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
14 oWote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
15 pWale waniambiao, “Aha! Aha!”
wafadhaishwe na iwe aibu yao.
16 qLakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
Bwana atukuzwe!”

17 rLakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Bwana na anifikirie.
Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu;
Ee Mungu wangu, usikawie.
Copyright information for SwhNEN