Psalms 44:1-4
Kuomba Ulinzi Wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora.
1 aEe Mungu, tumesikia kwa masikio yetu,baba zetu wametueleza
yale uliyotenda katika siku zao,
siku za kale.
2 bKwa mkono wako uliwafukuza mataifa
na ukawapanda baba zetu,
uliangamiza mataifa
na kuwastawisha baba zetu.
3 cSio kwa upanga wao waliipata nchi,
wala si mkono wao uliwapatia ushindi;
ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume,
na nuru ya uso wako,
kwa kuwa uliwapenda.
4 dWewe ni mfalme wangu na Mungu wangu,
unayeamuru ushindi kwa Yakobo.
Copyright information for
SwhNEN