Psalms 45
Wimbo Wa Arusi Ya Kifalme
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Yungiyungi.” Utenzi wa wana wa Kora. Wimbo wa arusi.
1Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jemaninapomsimulia mfalme mabeti yangu;
ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.
2 aWewe ni bora kuliko watu wengine wote
na midomo yako imepakwa neema,
kwa kuwa Mungu amekubariki milele.
3 bJifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu,
jivike fahari na utukufu.
4 cKatika fahari yako, songa mbele kwa ushindi,
kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki,
mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha.
5 dMishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme,
mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako.
6 eEe Mungu, kiti chako cha enzi
kitadumu milele na milele,
fimbo ya utawala wa haki
itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako.
7 fUnaipenda haki na kuchukia uovu;
kwa hiyo Mungu, Mungu wako,
amekuweka juu ya wenzako,
kwa kukupaka mafuta ya furaha.
8 gMavazi yako yote yana harufu nzuri
ya manemane, udi na mdalasini;
kutoka kwenye majumba ya kifalme
yaliyopambwa kwa pembe za ndovu,
sauti za vinanda vya nyuzi
zinakufanya ufurahi.
9 hBinti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa;
kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri.
10 iSikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio:
Sahau watu wako na nyumba ya baba yako.
11 jMfalme ameshangazwa na uzuri wako;
mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako.
12 kBinti wa Tiro atakuletea zawadi,
watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako.
13 lUtukufu wote una binti mfalme katika chumba chake;
vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu.
14 mAnaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa,
mabikira wenzake wanamfuata
na wanaletwa kwako.
15 nWanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha,
na kuingia katika jumba la mfalme.
16 oWana wenu watachukua nafasi za baba zenu,
mtawafanya wakuu katika nchi yote.
17 pNitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote,
kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele.
Copyright information for
SwhNEN