Psalms 55
Maombi Ya Mtu Aliyesalitiwa Na Rafiki
Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi.
1 aEe Mungu, sikiliza maombi yangu,wala usidharau hoja yangu.
2 bNisikie na unijibu.
Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa
3 ckwa sauti ya adui,
kwa kukaziwa macho na waovu,
kwa sababu wananiletea mateso juu yangu
na kunitukana kwa hasira zao.
4 dMoyo wangu umejaa uchungu,
hofu ya kifo imenishambulia.
5 eWoga na kutetemeka vimenizunguka,
hofu kuu imenigharikisha.
6Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa!
Ningeruka niende mbali kupumzika.
7 fNingalitorokea mbali sana
na kukaa jangwani,
8 gningaliharakisha kwenda mahali pa salama,
mbali na tufani kali na dhoruba.”
9 hEe Bwana, uwatahayarishe waovu
na uwachanganyishie semi zao,
maana nimeona jeuri na ugomvi mjini.
10 iUsiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake,
uovu na dhuluma vimo ndani yake.
11 jNguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini,
vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake.
12Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia,
kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu,
ningejificha asinione.
13 kKumbe ni wewe, mwenzangu,
mshiriki na rafiki yangu wa karibu,
14 lambaye awali tulifurahia ushirika mzuri,
tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.
15 mKifo na kiwajie adui zangu ghafula,
na washuke kuzimu wangali hai,
kwa maana uovu upo ndani yao.
16Lakini ninamwita Mungu,
naye Bwana huniokoa.
17 nJioni, asubuhi na adhuhuri
ninalia kwa huzuni,
naye husikia sauti yangu.
18 oHuniokoa nikawa salama katika vita
vilivyopangwa dhidi yangu,
ingawa watu wengi hunipinga.
19 pMungu anayemiliki milele,
atawasikia na kuwaadhibu,
watu ambao hawabadilishi njia zao,
wala hawana hofu ya Mungu.
20 qMwenzangu hushambulia rafiki zake,
naye huvunja agano lake.
21 rMazungumzo yake ni laini kama siagi,
hata hivyo vita vimo moyoni mwake.
Maneno yake ni mororo kuliko mafuta,
hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.
22 sMtwike Bwana fadhaa zako,
naye atakutegemeza,
hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
23 tLakini wewe, Ee Mungu,
utawashusha waovu katika shimo la uharibifu.
Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila,
hawataishi nusu ya siku zao.
Lakini mimi ninakutumaini wewe.
Copyright information for
SwhNEN