Psalms 76
Mungu Wa Israeli Ni Mhukumu Wa Dunia Yote
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1 aKatika Yuda, Mungu anajulikana,jina lake ni kuu katika Israeli.
2 bHema lake liko Salemu,
makao yake katika Sayuni.
3 cHuko alivunja mishale imetametayo,
ngao na panga, silaha za vita.
4 dWewe unangʼaa kwa mwanga,
mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori.
5 eMashujaa hulala wametekwa nyara,
hulala usingizi wao wa mwisho;
hakuna hata mmoja wa watu wa vita
anayeweza kuinua mikono yake.
6 fKwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,
farasi na gari la vita vilikaa kimya.
7 gWewe peke yako ndiye wa kuogopwa.
Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika?
8 hKutoka mbinguni ulitamka hukumu,
nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya:
9 iwakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu,
kuwaokoa wote walioonewa katika nchi.
10 jHakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa,
na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi.
11 kWekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza;
nchi zote za jirani na walete zawadi
kwa Yule astahiliye kuogopwa.
12Huvunja roho za watawala;
anaogopwa na wafalme wa dunia.
Copyright information for
SwhNEN