Psalms 80
Maombi Kwa Ajili Ya Kuponywa Kwa Taifa
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano.” Zaburi ya Asafu.
1 aEe Mchungaji wa Israeli tusikie,wewe umwongozaye Yosefu kama kundi;
wewe uketiye katika kiti cha enzi
katikati ya makerubi, angaza
2 bmbele ya Efraimu, Benyamini na Manase.
Uamshe nguvu zako,
uje utuokoe.
3 cEe Mungu, uturejeshe,
utuangazie uso wako,
ili tuweze kuokolewa.
4 dEe Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote,
hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi
dhidi ya maombi ya watu wako?
5 eUmewalisha kwa mkate wa machozi,
umewafanya wanywe machozi bakuli tele.
6 fTumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu,
na adui zetu wanatudhihaki.
7 gEe Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;
utuangazie uso wako,
nasi tuweze kuokolewa.
8 hUlileta mzabibu kutoka Misri,
ukawafukuza mataifa, ukaupanda.
9Uliandaa shamba kwa ajili yake,
mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.
10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,
matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.
11 iMatawi yake yalienea mpaka Baharini, ▼
▼Huenda inamaanisha Bahari ya Mediterania.
machipukizi yake mpaka kwenye Mto. ▼
▼Yaani Mto Frati.
12 lMbona umebomoa kuta zake
ili wote wapitao karibu
wazichume zabibu zake?
13 mNguruwe mwitu wanauharibu
na wanyama wa kondeni hujilisha humo.
14 nTurudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote!
Tazama chini kutoka mbinguni na uone!
Linda mzabibu huu,
15 omche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume,
mwana uliyemlea
kwa ajili yako mwenyewe.
16 pMzabibu wako umekatwa, umechomwa moto,
unapowakemea, watu wako huangamia.
17 qMkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume,
mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
18 rNdipo hatutakuacha tena,
utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako.
19 sEe Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;
utuangazie uso wako,
ili tuweze kuokolewa.
Copyright information for
SwhNEN