Psalms 81
Wimbo Wa Sikukuu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu.
1 aMwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu;mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo!
2 bAnzeni wimbo, pigeni matari,
pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.
3 cPigeni baragumu za pembe za kondoo dume
wakati wa Mwandamo wa Mwezi,
na wakati wa mwezi mpevu,
katika siku ya Sikukuu yetu;
4 dhii ni amri kwa Israeli,
agizo la Mungu wa Yakobo.
5 eAliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu
alipotoka dhidi ya Misri,
huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa.
6 fAsema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao;
mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu.
7 gKatika shida yako uliniita nami nikakuokoa,
nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo;
nilikujaribu katika maji ya Meriba.
8 h“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya:
laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!
9 iHamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu;
msimsujudie mungu wa kigeni.
10 jMimi ni Bwana Mungu wako,
niliyekutoa nchi ya Misri.
Panua sana kinywa chako
nami nitakijaza.
11 k“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza;
Israeli hakutaka kunitii.
12 lBasi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao
wafuate mashauri yao wenyewe.
13 m“Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza,
kama Israeli wangalifuata njia zangu,
14 nningaliwatiisha adui zao kwa haraka,
na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao!
15 oWale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake,
na adhabu yao ingedumu milele.
16 pBali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora,
na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”
Copyright information for
SwhNEN