Psalms 82
Maombi Kwa Ajili Ya Kutaka Haki
Zaburi ya Asafu.
1 aMungu anaongoza kusanyiko kuu,anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:
2 b“Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki
na kuonyesha upendeleo kwa waovu?
3 cTeteeni wanyonge na yatima,
tunzeni haki za maskini na walioonewa.
4Mwokoeni mnyonge na mhitaji,
wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
5 d“Hawajui lolote, hawaelewi lolote.
Wanatembea gizani;
misingi yote ya dunia imetikisika.
6 e“Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;
ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’
7 fLakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;
mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”
8 gEe Mungu, inuka uihukumu nchi,
kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.
Copyright information for
SwhNEN