Psalms 92
Wimbo Wa Kumsifu Mungu
Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato.
1 aNi vyema kumshukuru Bwanana kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,
2 bkuutangaza upendo wako asubuhi,
na uaminifu wako wakati wa usiku,
3 ckwa zeze yenye nyuzi kumi
na kwa sauti ya kinubi.
4 dEe Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha,
nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.
5 eEe Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako,
tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!
6 fMjinga hafahamu,
mpumbavu haelewi,
7 gingawa waovu huchipua kama majani
na wote watendao mabaya wanastawi,
wataangamizwa milele.
8Bali wewe, Ee Bwana,
utatukuzwa milele.
9 hEe Bwana, hakika adui zako,
hakika adui zako wataangamia.
Wote watendao mabaya watatawanyika.
10 iUmeitukuza pembe ▼
▼Pembe inawakilisha nguvu.
yangu kama ile ya nyati dume,mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.
11 kMacho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa,
masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu.
12 lWenye haki watastawi kama mtende,
watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,
13 mwaliopandwa katika nyumba ya Bwana,
watastawi katika nyua za Mungu wetu.
14 nWakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,
watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,
15 owakitangaza, “Bwana ni mkamilifu;
yeye ni Mwamba wangu,
na ndani yake hamna uovu.”
Copyright information for
SwhNEN