Revelation of John 16:3-6
3 aMalaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.4 bMalaika wa tatu akalimwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikawa damu. 5 cNdipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema:
“Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa,
wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu,
kwa sababu umehukumu hivyo;
6 dkwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako
na manabii wako,
nawe umewapa damu wanywe
kama walivyostahili.”
Copyright information for
SwhNEN