Song of Solomon 6

Marafiki

1 aMpenzi wako amekwenda wapi,
ewe mzuri kupita wanawake wote?
Mpenzi wako amegeukia njia ipi,
tupate kumtafuta pamoja nawe?
Mpendwa

2 bMpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,
kwenye vitalu vya vikolezo,
kujilisha bustanini
na kukusanya yungiyungi.
3 cMimi ni wake mpenzi wangu,
na mpenzi wangu ni wangu;
yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.

Shairi La Tano

Mpenzi

4 dWewe ni mzuri, mpenzi wangu, kama Tirsa,
upendezaye kama Yerusalemu,
umetukuka kama jeshi lenye bendera.
5Uyageuze macho yako mbali nami,
yananigharikisha.
Nywele zako ni kama kundi la mbuzi
wanaoteremka kutoka Gileadi.
6Meno yako ni kama kundi la kondoo
watokao kuogeshwa.
Kila mmoja ana pacha lake,
hakuna hata mmoja aliye peke yake.
7 eMashavu yako nyuma ya shela yako
ni kama vipande viwili vya komamanga.
8 fPanaweza kuwepo malkia sitini,
masuria themanini
na mabikira wasiohesabika;
9 glakini hua wangu, mkamilifu wangu,
ni wa namna ya pekee,
binti pekee kwa mama yake,
kipenzi cha yeye aliyemzaa.
Wanawali walimwona na kumwita aliyebarikiwa;
malkia na masuria walimsifu.
Marafiki

10Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko,
mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,
ametukuka kama nyota zifuatanazo?
Mpenzi

11 hNiliteremka kwenye bustani ya miti ya milozi
ili kutazama machipuko ya bondeni,
kuona kama mizabibu imechipua
au kama mikomamanga imechanua maua.
12Kabla sijangʼamua,
shauku yangu iliniweka
katikati ya magari ya kifalme ya kukokotwa na farasi ya watu wangu.
Marafiki

13 iRudi, rudi, ee Mshulami;
rudi, rudi ili tupate kukutazama!
Mpenzi

Kwa nini kumtazama Mshulami,
kama kutazama ngoma ya Mahanaimu?
Mahanaimu hapa ina maana ya majeshi mawili.

Copyright information for SwhNEN