‏ Daniel 2:20-23

20 ana akasema: “Lihimidiwe jina la Mungu milele na milele;
hekima na uweza ni vyake.

21 bYeye hubadili nyakati na majira;
huwaweka wafalme na kuwaondoa.
Huwapa hekima wenye hekima,
na maarifa wenye ufahamu.

22 cHufunua siri na mambo yaliyofichika;
anajua yale yaliyo gizani,
nayo nuru hukaa kwake.

23 dNinakushukuru na kukuhimidi,
Ee Mungu wa baba zangu:
Umenipa hekima na uwezo,
umenijulisha kile tulichokuomba,
umetujulisha ndoto ya mfalme.”

Danieli Aifasiri Ndoto

Copyright information for SwhKC