1 Corinthians 1:10-12

10 aNawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi. 11 bNdugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu. 12 cMaana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo”; mwingine, “Mimi ni wa Apolo”; mwingine, “Mimi ni wa Kefa,”
Yaani Petro.
na mwingine, “Mimi ni wa Al-Masihi.”

Copyright information for SwhKC