‏ 1 Corinthians 12:4-9

4 aKuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule. 5 bKuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule. 6 cKisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

7 dBasi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote. 8 eMaana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo. 9 fMtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya kwa huyo Roho mmoja.
Copyright information for SwhKC