1 Corinthians 15:1-6
Kufufuka Kwa Al-Masihi
1 aBasi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama. 2 bKwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili. 3 cKwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Al-Masihi alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko, 4 dya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko, 5 ena kwamba alimtokea Kefa, ▼▼ Yaani Petro.
kisha akawatokea wale kumi na wawili. 6 gBaadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala.
Copyright information for
SwhKC