2 Chronicles 29:1-6

Hezekia Mfalme Wa Yuda

(2 Wafalme 18:1-12)

1 aHezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. 2 bAkafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Daudi baba yake alivyofanya.

3 cKatika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa utawala wa alifungua milango ya Hekalu la Bwana, na kuikarabati. 4Akawaingiza makuhani na Walawi ndani na kuwakutanisha katika uwanja upande wa mashariki 5 dna kusema: “Nisikilizeni mimi, enyi Walawi! Jitakaseni nafsi zenu sasa, mkaitakase na nyumba ya Bwana, Mungu wa baba zenu. Ondoeni uchafu wote kutoka mahali patakatifu. 6 eBaba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa Bwana Mwenyezi Mungu wetu na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya Bwana wakamgeuzia visogo vyao.
Copyright information for SwhKC