‏ 2 Corinthians 4:4-6

4 aKwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Al-Masihi, aliye sura ya Mungu. 5 bKwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Isa Al-Masihi kuwa ni Bwana na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Isa. 6 cKwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, “Nuru na ing’ae gizani,” ameifanya nuru yake ing’ae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Al-Masihi.

Copyright information for SwhKC