2 Samuel 22:2-7
2 aAkasema: “Bwana ni mwamba wangu,ngome yangu na mwokozi wangu,
3 bMungu wangu ni mwamba wangu,
ambaye kwake ninakimbilia,
ngao yangu na pembe ya wokovu wangu.
Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu
na mwokozi wangu,
huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.
4 cNinamwita Bwana, anayestahili kusifiwa,
nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
5 d“Mawimbi ya mauti yalinizunguka,
mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
6 eKamba za kuzimu ▼
▼ Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, maana yake ni Shimo lisilo na mwisho.
zilinizunguka,mitego ya mauti ilinikabili.
7 gKatika shida yangu nalimwita Bwana,
nilimlilia Mungu wangu.
Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu,
kilio changu kikafika masikioni mwake.
Copyright information for
SwhKC