2 Samuel 22:21-25


21 aBwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.

22 bKwa maana nimezishika njia za Bwana;
sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.

23 cSheria zake zote zi mbele yangu,
wala sijayaacha maagizo yake.

24 dNimekuwa sina hatia mbele zake,
nami nimejilinda nisitende dhambi.

25 e Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu,
sawasawa na usafi wangu machoni pake.

Copyright information for SwhKC