Acts 1:1-6

(1:1–5:42)

Ahadi Ya Roho Mtakatifu

1 aKatika kitabu changu cha kwanza nilikuandikia, mpendwa Theofilo, kuhusu mambo yote Isa aliyofanya na kufundisha tangu mwanzo, 2 bhadi siku ile alipochukuliwa kwenda mbinguni, baada ya kuwapa maagizo kupitia kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua. 3 cBaada ya mateso yake, alijionyesha kwao na kuwathibitishia kwa njia nyingi kwamba yeye yu hai. Katika muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake aliwatokea na kunena kuhusu Ufalme wa Mungu. 4 dWakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake. 5 eYahya aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Isa Apaa Mbinguni

(Marko 16:19-20; Luka 24:50-53)

6 fMitume walipokuwa wamekusanyika pamoja, wakamuuliza Isa, “Bwana, je, huu ndio wakati wa kuwarudishia Israeli ufalme?”

Copyright information for SwhKC