Acts 1:14-16

14 aHawa wote waliungana pamoja katika maombi. Pamoja nao walikuwepo wanawake kadha, na Mariamu mama yake Isa, pamoja na ndugu zake Isa.

15 bKatika siku hizo Petro akasimama katikati ya waumini (jumla yao wote walikuwa watu wapatao 120), akasema, 16 c“Ndugu zangu, ilibidi Andiko litimie ambalo Roho Mtakatifu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda aliyewaongoza wale waliomkamata Isa.
Copyright information for SwhKC