‏ Acts 16:1-6

Timotheo Aungana Na Paulo Na Sila

1 aPaulo akafika Derbe na kisha Listra, ambako kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, ambaye mama yake alikuwa Myahudi aliyeamini, lakini baba yake alikuwa Myunani. 2 bAlikuwa amesifiwa sana na wale ndugu waliokuwa wameamini huko Listra na Ikonio 3 cPaulo alitaka Timotheo afuatane naye, hivyo akamchukua na kumtahiri kwa sababu ya Wayahudi waliokuwa wanaishi eneo lile kwa maana wote walimjua baba yake ni Myunani. 4 dWalipokuwa wakienda mji kwa mji, wakawa wanawapa maamuzi yaliyotolewa na mitume na wazee huko Yerusalemu ili wayafuate. 5 eHivyo makanisa yakawa imara katika imani na kuongezeka kiidadi kila siku.

6 fPaulo pamoja na wenzake wakasafiri sehemu za Frigia na Galatia, kwa kuwa Roho Mtakatifu hakuwaruhusu kulihubiri neno huko Asia.
Copyright information for SwhKC