Acts 2:1-6
Kushuka Kwa Roho Mtakatifu
1 aSiku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja. 2 bGhafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3 cZikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. 4 dWote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia. 5 eBasi walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu. 6Waliposikia sauti hii, umati wa watu ulikusanyika pamoja wakistaajabu, kwa sababu kila mmoja wao aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.
Copyright information for
SwhKC