Acts 9:1-6
Kuokoka Kwa Sauli
(Matendo 22:6-16; 26:12-18)
1 aWakati ule ule, Sauli alikuwa bado anazidisha vitisho vya kuua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, 2 bnaye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mtu yeyote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu. 3 cBasi akiwa katika safari yake, alipokaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ikamwangaza kotekote. 4 dAkaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona unanitesa?” 5 eSauli akajibu, “U nani wewe, Bwana?” Ile sauti ikajibu, “Mimi ni Isa unayemtesa.” 6 f“Sasa inuka uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.”
Copyright information for
SwhKC