Deuteronomy 1:1-6

Amri Ya Kuondoka Mlima Horebu

1 aHaya ni maneno Musa aliyoyasema kwa Israeli yote jangwani mashariki ya Yordani, ambayo iko Araba, inayokabiliana na Sufu, kati ya Parani na Tofeli, Labani, Haserothi na Dizahabu. 2 b(Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya Mlima Seiri mpaka Kadesh-Barnea.)

3 cKatika mwaka wa arobaini, siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na moja, Musa aliwatangazia Waisraeli yale yote Bwana aliyomwamuru kuwahusu. 4 dHii ilikuwa baada ya kumshinda Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni, na pia huko Edrei alikuwa amemshinda Ogu mfalme wa Bashani, ambaye alitawala huko Ashtarothi. 5 eHuko mashariki ya Yordani katika nchi ya Moabu, Musa alianza kuielezea sheria hii, akisema:

6 f Bwana Mwenyezi Mungu wetu alisema nasi huko Horebu, “Mmekaa vya kutosha katika mlima huu.
Copyright information for SwhKC