Deuteronomy 19:1-6

Miji Ya Makimbilio

(Hesabu 35:9-34; Yoshua 20:1-9)

1 aWakati Bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapokuwa amewaangamiza mataifa ambayo nchi yao anawapa ninyi, wakati mtakapokuwa mmewafukuza na kuishi katika miji yao na nyumba zao, 2 bndipo mtenge miji mitatu iliyopo katikati ya nchi kwa ajili yenu, katika nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa kuimiliki. 3Jengeni barabara katika miji hiyo na kuigawa mara tatu, nchi anayowapa Bwana Mwenyezi Mungu wenu kama urithi, ili kwamba yeyote amuuaye mtu aweze kukimbilia humo.

4Hii ndiyo kanuni kuhusu mtu amuuaye mwingine na kukimbilia humo kuokoa maisha yake, yaani, yeye amuuaye jirani yake bila kukusudia, wala hakumchukia kabla ya hapo. 5Kwa mfano, mtu aweza kwenda msituni na jirani yake kukata miti, naye anapozungusha shoka kuangusha mti, shoka linaweza kuchomoka kutoka kwenye mpini na kumpiga jirani yake na kumuua. Yule mtu anaweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake. 6 cKama sivyo, mlipiza kisasi cha damu anaweza kumfuatilia kwa hasira kali, naye akamkamata na kumuua kama umbali ni mrefu sana hata ingawa hastahili kifo, kwa sababu amemuua jirani yake bila kukusudia.
Copyright information for SwhKC