Exodus 15:1-6

Wimbo Wa Musa Na Miriamu

1 aNdipo Musa na Waisraeli wakamwimbia Bwana wimbo huu: “Nitamwimbia Bwana,
kwa kuwa ametukuzwa sana.
Farasi na mpanda farasi
amewatosa baharini.

2 b Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu;
amekuwa wokovu wangu.
Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu,
Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.

3 c Bwana ni shujaa wa vita;
Bwana ndilo jina lake.

4 dMagari ya vita ya Farao na jeshi lake
amewatosa baharini.
Maafisa wa Farao walio bora sana
wamezamishwa katika Bahari ya Shamu.

5 eMaji yenye kina yamewafunika,
wamezama mpaka vilindini kama jiwe.


6 f“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana
ulitukuka kwa uweza.
Mkono wako wa kuume, Ee Bwana,
ukamponda adui.
Copyright information for SwhKC