Exodus 24:15-18

15 aMusa alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, 16 bnao utukufu wa Bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Bwana akamwita Musa kutoka katikati ya lile wingu. 17 cKwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. 18 dKisha Musa akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana.
Copyright information for SwhKC