Exodus 25:1-6

Sadaka Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu

(Kutoka 35:4-9)

1 a Bwana akamwambia Musa, 2“Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa niaba yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa. 3Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: dhahabu, fedha na shaba; 4 bnyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; singa za mbuzi; 5 cngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;
Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.
mbao za mshita;
6 emafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri;
Copyright information for SwhKC