Exodus 27:20-21

20 a“Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake mfululizo. 21 bKatika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Haruni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za Bwana. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo.
Copyright information for SwhKC