Exodus 37:10-15

10 aAkatengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,
Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.
upana wa dhiraa moja,
Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45.
na kimo cha dhiraa moja na nusu.
11Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 12Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,
Nyanda nne ni sawa na sentimita 8.
na kuufanyia ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote.
13Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 14 ePete hizo ziliwekwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. 15Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu.
Copyright information for SwhKC