Exodus 7:13-15

13 aHata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Musa na Haruni, sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa amesema.

Pigo La Kwanza: Damu

14 bKisha Bwana akamwambia Musa, “Moyo wa Farao ni mgumu, anakataa kuwaachia watu kuondoka. 15Nenda kwa Farao asubuhi wakati anapokwenda mtoni. Ngoja ukingoni mwa Naili ili uonane naye, na uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka.
Copyright information for SwhKC