Exodus 7:8-13

8Bwana akamwambia Musa na Haruni, 9 a“Farao atakapowaambia, ‘Fanyeni muujiza,’ basi mwambie Haruni, ‘Chukua fimbo yako na uitupe chini mbele ya Farao,’ nayo fimbo itakuwa nyoka.”

10Ndipo Musa na Haruni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile Bwana alivyoagiza. Haruni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka. 11 bFarao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao. 12Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Haruni ikazimeza zile fimbo zao. 13 cHata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Musa na Haruni, sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa amesema.

Pigo La Kwanza: Damu

Copyright information for SwhKC