Ezekiel 30:1-6

Maombolezo Kwa Ajili Ya Misri

1Neno la Bwana likanijia kusema: 2 a“Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,
“Ole wa siku ile!”

3 bKwa kuwa siku ile imekaribia,
siku ya Bwana imekaribia,
siku ya mawingu,
siku ya maangamizi kwa mataifa.

4 cUpanga utakuja dhidi ya Misri,
nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.
Mauaji yatakapoangukia Misri,
utajiri wake utachukuliwa
na misingi yake itabomolewa.

5 dKushi
Kushi ndiyo Ethiopia.
na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya
Libya ndiyo Kubu.
na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

6 g“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka
na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.
Kutoka Migdoli hadi Aswani,
watauawa ndani yake kwa upanga,
asema Bwana Mwenyezi.

Copyright information for SwhKC