a Za 89:11; 90:2; 96:5; 102:25; Mit 8:23; Isa 40:21; 42:5; 51:13; 41:4, 26; Yn 1:1-2; Mwa 2:3; 14:19; Neh 9:6; Ay 9:8; 37:18; Yer 10:12; 32:17; 51:15; 2Fal 19:15; Mdo 14:15; 7:24; Efe 3:9; Kol 1:16; Ebr 1:10; 3:4; 11:3; Ufu 4:11; 10:6
Genesis 1:1-6
Siku Sita Za Uumbaji Na Sabato
1 aHapo mwanzo Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na dunia.2 bWakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mwenyezi Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.
3 cMwenyezi Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. 4 dMwenyezi Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mwenyezi Mungu akatenganisha nuru na giza. 5 eMwenyezi Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6 fMwenyezi Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.”
Copyright information for
SwhKC