‏ Genesis 1:3-8

3 aMwenyezi Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. 4 bMwenyezi Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mwenyezi Mungu akatenganisha nuru na giza. 5 cMwenyezi Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6 dMwenyezi Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.” 7 eKwa hiyo Mwenyezi Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo. 8 fMwenyezi Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.
Copyright information for SwhKC