Genesis 7:6-11

6 aNuhu alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia. 7 bNuhu na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika. 8Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vitambaavyo, 9 cwa kiume na wa kike, walikuja kwa Nuhu wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Nuhu. 10Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia.

11 dKatika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Nuhu, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa.
Copyright information for SwhKC