Habakkuk 1:2-4

Lalamiko La Habakuki


2 aEe Bwana, hata lini nitakuomba msaada,
lakini wewe husikilizi?
Au kukulilia, “Udhalimu!”
Lakini hutaki kuokoa?

3 bKwa nini unanifanya nitazame dhuluma?
Kwa nini unavumilia makosa?
Uharibifu na udhalimu viko mbele yangu;
kuna mabishano na mapambano kwa wingi.

4 cKwa hiyo sheria imepotoshwa,
nayo haki haipo kabisa.
Waovu wanawazunguka wenye haki,
kwa hiyo haki imepotoshwa.
Copyright information for SwhKC