Hebrews 7:2-7

2naye Ibrahimu alimpa sehemu ya kumi
Sehemu ya kumi mahali pengine huitwa fungu la kumi au zaka; sehemu ya kumi ya pato hutolewa kwa Mungu.
ya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “mfalme wa haki.” Na pia “mfalme wa Salemu” maana yake ni “mfalme wa amani.”
3 bHana Baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake. Kama Mwana wa Mungu, yeye adumu akiwa kuhani milele.

4 cTazama jinsi alivyokuwa mkuu: Hata Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. 5 dBasi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Ibrahimu. 6 eHuyu Melkizedeki, ingawa hakufuatia ukoo wake kutoka kwa Lawi, lakini alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Ibrahimu na kumbariki yeye aliyekuwa na zile ahadi. 7Wala hakuna shaka kwamba mdogo hubarikiwa na aliye mkuu kumliko yeye.
Copyright information for SwhKC