Isaiah 11:1-6

Tawi Kutoka Kwa Yese


1 aChipukizi litatokea kutoka shina la Yese,
kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.

2 bRoho wa Bwana atakaa juu yake,
Roho wa hekima na wa ufahamu,
Roho wa shauri na wa uweza,
Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana

3 cnaye atafurahia kumcha Bwana.

Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,
wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,

4 dbali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,
kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.
Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,
kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.

5 eHaki itakuwa mkanda wake
na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.


6 fMbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,
naye chui atalala pamoja na mbuzi,
ndama, mwana simba na ng’ombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja,
naye mtoto mdogo atawaongoza.
Copyright information for SwhKC