Isaiah 11:6-9


6 aMbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,
naye chui atalala pamoja na mbuzi,
ndama, mwana simba na ng’ombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja,
naye mtoto mdogo atawaongoza.

7 bNg’ombe na dubu watalisha pamoja,
watoto wao watalala pamoja,
na simba atakula majani makavu kama maksai.

8 cMtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka,
naye mtoto mdogo ataweka mkono wake
kwenye kiota cha fira.

9 dHawatadhuru wala kuharibu
juu ya mlima wangu mtakatifu wote,
kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwana
kama maji yajazavyo bahari.

Copyright information for SwhKC