Isaiah 43:3-8


3 aKwa kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako.
Ninaitoa Misri kuwa fidia yako,
Kushi na Seba badala yako.

4 bKwa kuwa wewe ni wa thamani na wa kuheshimiwa machoni pangu,
nami kwa kuwa ninakupenda,
nitatoa watu badala yako
na mataifa badala ya maisha yako.

5 cUsiogope, kwa kuwa mimi nipo pamoja nawe,
nitawaleta watoto wako kutoka mashariki,
na kukukusanya kutoka magharibi.

6 dNitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’
nayo kusini, ‘Usiwazuie.’
Walete wana wangu kutoka mbali,
na binti zangu kutoka miisho ya dunia:

7 ekila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu,
niliyemuumba kwa utukufu wangu,
niliyemhuluku na kumfanya.”

8 fUwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni,
wenye masikio lakini hawasikii.
Copyright information for SwhKC