Isaiah 49:1-6

Mtumishi Wa Bwana


1 aNisikilizeni, enyi visiwa, sikieni hili,
ninyi mataifa mlio mbali:
Kabla sijazaliwa, Bwana aliniita,
tangu kuzaliwa kwangu, amelitaja jina langu.

2 bAkafanya kinywa changu kuwa kama upanga ulionolewa,
katika uvuli wa mkono wake akanificha;
akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa,
na kunificha katika podo lake.

3 cAkaniambia, “Wewe u mtumishi wangu,
Israeli, ambaye katika yeye
nitaonyesha utukufu wangu.”

4 dLakini nilisema, “Nimetumika bure,
nimetumia nguvu zangu bure bila faida.
Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa Bwana,
nao ujira wangu uko kwa Mungu wangu.”


5 eSasa Bwana asema:
yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake,
kumrudisha tena Yakobo kwake
na kumkusanyia Israeli,
kwa maana nimepata heshima machoni pa Bwana,
naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;

6 fyeye asema:
“Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu
ili kurejeza makabila ya Yakobo,
na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi?
Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu wa Mataifa,
ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”

Copyright information for SwhKC