Jeremiah 1:1-6

1 aManeno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini. 2Neno la Bwana lilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, 3 bna pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.

Wito Wa Yeremia

4Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5 c“Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;
kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;
nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”

6 dNami nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.”

Copyright information for SwhKC