Jeremiah 10:1-6

Mungu Na Sanamu

1Sikieni lile ambalo Bwana, anena nanyi ee nyumba ya Israeli. 2 aHili ndilo asemalo Bwana: “Usijifunze njia za mataifa
wala usitishwe na ishara katika anga,
ingawa mataifa yanatishwa nazo.

3 bKwa maana desturi za mataifa hazina maana,
wanakata mti msituni,
na fundi anauchonga kwa patasi.

4 cWanaparemba kwa fedha na dhahabu,
wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike.

5 dSanamu zao ni kama sanamu
iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege
nazo haziwezi kuongea;
sharti zibebwe
sababu haziwezi kutembea.
Usiziogope; haziwezi kudhuru,
wala kutenda lolote jema.”


6 eHakuna aliye kama wewe, Ee Bwana;
wewe ni mkuu,
jina lako ni lenye nguvu katika uweza.
Copyright information for SwhKC