‏ Jeremiah 23:3-6

3 a“Mimi mwenyewe nitayakusanya mabaki ya kundi langu kutoka nchi zote ambazo nimewafukuzia, nami nitawarudisha katika malisho yao, mahali ambapo watazaa na kuongezeka idadi yao. 4 bNitaweka wachungaji juu yao ambao watawachunga, nao hawataogopa tena au kutishwa, wala hatapotea hata mmoja,” asema Bwana.
5 c Bwana asema, “Siku zinakuja,
nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki,
Mfalme atakayetawala kwa hekima,
na kutenda lililo haki na sawa katika nchi.

6 dKatika siku zake, Yuda ataokolewa
na Israeli ataishi salama.
Hili ndilo jina atakaloitwa:
Bwana Haki Yetu.

Copyright information for SwhKC