Jeremiah 49:7-12

7 aKuhusu Edomu:

Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Je, hakuna tena hekima katika Temani?
Je, shauri limewapotea wenye busara?
Je, hekima yao imechakaa?

8 bGeuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,
wewe uishiye Dedani,
kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esau
wakati nitakapomwadhibu.

9 Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako,
wasingebakiza zabibu chache?
Kama wezi wangekujia usiku,
je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?

10 cLakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,
nitayafunua maficho yake,
ili asiweze kujificha.
Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,
naye hatakuwepo tena.

11 dWaache yatima wako; nitayalinda maisha yao.
Wajane wako pia
wanaweza kunitumaini mimi.”

12 eHili ndilo asemalo Bwana: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe.
Copyright information for SwhKC