Job 18:11-16
11 aVitisho vimemtia hofu kila upande,
na adui zake humwandama kila hatua.
12 bJanga linamwonea shauku;
maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.
13 cNayo yatakula sehemu ya ngozi yake;
mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.
14 dAtang’olewa kutoka usalama wa hema lake,
na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.
15 eMoto utakaa katika hema lake;
moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.
16 fMizizi yake chini itakauka
na matawi yake juu yatanyauka.
Copyright information for
SwhKC